VERSE-1 Najua hiki ndo kipindi ukipendacho, Najua sasa hivi upo karibu na radio yako, Labda peke yako au na rafiki zako, Naomba kidogo ongeza sauti ya radio, Nachukua nafasi kuongea nawe kwa wimbo (huu, uuuuh uuuuh uuuh) Nimetunga special kwa ajili yako mrembo (uuuh, uuuuh uuuuh uuuuh) Mtangazaji kati ya wimbo usiweke jingo (uuuuh, uuuuh uuuuh uuuuh) Nimetunga rasmi kwa mtu aliye single (uuuuh, aliye single uuuh) CHORUS Kwa ajili yako naimba, Sauti hiii sikia, Habari hii pokea, Zingatia mrembo, usipuze mrembo (2x) Zingatia aaaah, zingatia ahaaaaa VERSE-2 Ndani ya roho yangu uko pekeyako, Usihofu mummy hakuna mwenzako, Nimezaliwa mimi kwa ajili yako, Naahidi sitotupa penzi lako, Nimekupa nafasi kubwa ndani ya moyo,uuuh uuuuh uuuh Ruksa tu niite baba watoto wako, uuuh uuuuh uuuh Kipingamizi hakuna juu yako, uuuh uuuuh uuuh Come closer nipunguze mapigo ya moyo, CHORUS Kwa ajili yako naimba, Sauti hiii sikia, Habari hii pokea, Zingatia mrembo, usipuze mrembo (2x) Zingatia aaaah, zingatia ahaaaaa VERSE-3 Moyo wangu unatamani sana, mimi kuwa na wewe Acha niseme hadharani ,kila mtu asikie Moyo wangu unatamani sana, mimi kuwa na wewe Acha niseme hadharani ,kila mtu asikie Asali ni tamu baby kwa anayefahamu, Ila ni chungu sana kwa asiyefahamu, Sogea karibu yangu, tulia kabisa, Lala kifuani kwangu, sinzia kabisa CHORUS Kwa ajili yako naimba, Sauti hiii sikia, Habari hii pokea, Zingatia mrembo, usipuuze mrembo (2x) Zingatia aaaah, zingatia ahaaaaa © Hussein Machozi